Mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Rais Samia afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu

Rais wa Tanzani Samia Suluhu amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya.

Akitangaza mabadiliko hayo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia ''ameunganisha wizara tatu, iliyokuwa wizara ya uwekezaji iliyokuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na pia ameunganisha wizara ya biashara moja ambayo itaitwa uwekezaji , viwanda na biashara'', amesema Balozi Hussein Kattanga.

Aidha kama alivyoahidi Rais Samia ameunda Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia ,wanawake na Makundi maalum.

Amefanya pia mabadiliko katika wizara ya afya.

Wizara maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, wizara hii itaaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima ambaye alikua waziri wa Afya.

CHANZO CHA PICHA,WIZARA YA AFYA

Maelezo ya picha,

Wizara mpya ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, itaaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima ambaye alikua waziri wa Afya.

Kilichojitokeza zaidi katika mabadiliko baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia ni kuundwa kwa Wizara Mpya ambayo ni Wizara maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, wizara hii itaaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima ambaye alikua waziri wa Afya.

Wizara ya afya sasa itaongozwa na Ole Mollel.

Kulingana na mabadiliko hayo, Wizara ya katiba na sheria imepata waziri mpya George Simbachawene ambaye amechukua wadhifa wa Profesa Palamagamba Kabudi.

Wizara ya Habari na teknolojia ya habari pia itaongozwa na Waziri mpya aliyekuwa Waziri wa zamani Nape Moses Nnauye.

Kulingana na Balozi Kattanga, Rais Samia amefanya mabadiliko pia katika nafasi za makatibu wakuu na Manaibu katibu wakuu.

Amteua Bw Hamad Yusuf Masauni kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi . Bw Masauni alikuwa Naibu waziri Wizara ya fedha.

Amemteua Dkt Pindi Chana kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu atakeyshugulikia masuala ya sera Bunge na uratibau.

Wengine ni Dkt Angelina Mabula aliyekuwa Naibu waziri wa Wizara ya ardhi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya kazi.

Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri Tanzania - wanne watupwa, tisa wabadilishwa wizara

Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaongozwa na Waziri mpya Jenista Mhagama ambaye amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu.

Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa atakuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Kuchukua nafasi ya Inocent Bashungwa.

Innocent Bashungwa, anakuwa Waziri mpya wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ummy Mwalimu, aliyehamishiwa Wizara ya Afya.

Aliyekuwa Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima sasa nataongoza wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watu wenye mahitaji maalum.

Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Pindi Chana sasa ameteuliwa kuongoza Wizara ya Sera na Bunge katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mwingine Katika Ofisi ya Waziri Mkuu ni Profesa Joyce Ndalichako atakayeshugulika na Kazi na Ajira ambaye amehamishwa kutoka Wizara ya Elimu, Syansi na Teknolojia.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi sasa itaongozwa na Masauni Yusuph Masauni aliyepandishwa wadhifa kutoka Naibu waziri na anachukua nafasi ya Simbachawene, aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

Simbachawene anachukua nafasi ya Prof. Palamagamba Kabudi ambaye ameachwa nje ya baraza.

Pia Aliyekuwa Naibu waziri wa Kilimo, Husseon Bashe sasa anakuwa waziri kamili akichukua nafasi ya Profesa Adolf Mkenda aliyehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Naibu waziri mwingine aliyepandishwa cheo ni Agelina Mabula atakayeongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi kuchukua nafasi ya William Lukuvi, mwanasiasa mkongwe aliyedumu katika nafasi za juu serikali kwa muda mrefu na pia ni mbunge wa Ismani mkoani Iringa kwa zaidi ya miaka 25.

Dkt. Ashatu Kijaji sasa ni Waziri mpya wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara akihamishwa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na anachukua nafasi ya Prof. Kitila Mkubo na Geoffrey Mwambe(Uwekezaji) ambao wameachwa nje baraza jipya.

Nape Nnauye ndiye Waziri mpya wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, alikotoka Dkt Kijaji. Nape aliwahi kuongoza Wizara ya Habari na kuondolewa mwaka 2017 na Rais John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Mawaziri waliobakia katika nafasi zao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberatha Mulamula; Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri wa Nishati, January Mkamba; Waziri wa Madini, Doto Biteko; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro; Waziri wa Maji, Jumaa Aweso; Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa; Waziri wa Ulinzi, Stegomena Tax; na Waziri Ofisi ya Rais - Kazi Maaalum, George Mkuchika.

Majina mapya katika baraza la mawaziri la Samia

Majina mapya yaliyoingia katika wizara hizi ni pamoja na ya mawaziri kamili Nape Nnauye, Pindi Chana na Hamad Masauni, Angelina Mabula na Hussein Bashe.

Ridhiwani

CHANZO CHA PICHA,RIDHIWANI KIKWETE/FACEBOOK

Maelezo ya picha,

Ridhiwani Kikwete, ni miongoni mwa sura mpya zilizoingia katika baraza la mawaziri la Rais Samia Suluhu

Kwa upande wa manaibu Ridhiwani Kikwete ameteuliwa kuwa naibu waziri wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi. Antony Mavunde Naibu wizara ya kilimo, Jumanne Sagini naibu waziri wizara ya mambo ya ndani. Lemomo Kiruswa ambaye ni naibu waziri wa Madini, na Atupele Mwakibete naibu waziri wizara ya ujenzi na uchukuzi.

Mabadiliko haya ya baraza la mawaziri nchini Tanzania yanajiri siku chache baada ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai kujiuzulu wadhifa huo, Alhamisi tarehe 6 Januari 2022.

Kwa mujibu wa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

"Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa bunge la Jamhuri ." ilisema sehemu ya taarifa hiyo na

Hatua ya kujiuzulu kwake ilijiri baada ya kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa viongozi mbali mbali ndani ya chama cha CCM kumtaka Ndugai kujiuzulu baada ya majibizano kati yake na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu serikali kuchukua mikopo ya maendeleo. Rais Samia tayari alijitokeza na kusema kwamba kauli za Ndugai huenda zinachochewa na hofu za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 .

Source: BBC







Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment