Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga akitoa maelezo jinsi kiwanda hicho
kinavyofanya kazi zake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (kushoto), Mwakilishi
Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (kulia) pamoja na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto kukagua miradi
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. (Picha na Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
Kutoratibiwa
kwa mbegu za alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto
kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika
kuendesha viwanda vyao kwa gharama nafuu.
Hayo
yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus
Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro
Rodriguez.
Mratibu
huyo alikuwa Dodoma kwa shughuli mbalimbali za ukaguzi wa miradi pamoja
na kuhudhuria shughuli za bunge la Tanzania lililomalizika jana.
Timothy
alisema kwamba pamoja kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa mbegu za kutosha
nchini Tanzania,hali halisi inayoelezwa na wasindikaji inaashiria kwamba
sekta hairatibiwi vyema kwani wasindikaji hukaa muda mrefu bila kuwa na
mbegu za kusindika.
Aidha
alisema kwamba mbegu za alizeti zinazovunwa kuanzia Aprili hadi Julai na
huwa na bei nafuu kipindi hicho lakini kama wasindikaji wakikosa mitaji
na kununua mbegu chache, msimu unapoisha hawawezi tena kuendelea
kufungua viwanda vyao.
Alisema
kwamba wasindikaji hao wanakumbana na kiwango kikubwa cha riba kuanzia
asilimia 20 kwenda juu , riba ambayo inakwamisha maendeleo ya viwanda
hivyo.
Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia), Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa pili
kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum
(katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric
Otto (wa pili kulia) wakipata picha ya ukumbusho katika matanki ya
kuhifadhia mafuta ya alizeti kiwandani hapo.
Hata
hivyo alipoulizwa wanafanya nini katika kusaidia wasindikaji hao
kukabiliana na hali hiyo alisema kwamba kupitia kongano hilo na
Shirikisho la wasindikaji wadogo wa alizeti kanda ya mashariki na kati
(CEZOSOPA). wana mipango ya kuwezesha wasindikaji hao kuwa na nguvu
katika soko na kuwa na uwezo wa kupata mitaji bila gharama kubwa.
Aidha
kupitia kongano hilo chama hicho kitawezeshwa uboreshwaji wa viwanda vya
wanachama wake ili viweze kushindana na kukidhi viwango vya Shirika la
Viwango nchini Tanzania (TBS).
Wakala
huyo alisema hayo katika mahojiano yaliyofanyika kufuatia ziara ya mradi
wa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez kwenye
kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya
Dodoma, kinachonufaika na mradi wa ubia wa uboreshaji viwanda kati ya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Wizara ya
Viwanda na Biashara (TIUMP).
Kwa
mujibu wa taarifa ya UNIDO, taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa inachangia
kuimarika kwa sekta ya viwanda vidogo na vya kati vya usindikaji mafuta
na kuviweka katika ushindani.
Aidha kupitia UNIDO ni viwanda hivyo vinawekwa katika hali ya kukua kuwa viwanda vikubwa.(P.T)
Mfanyakazi
wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Alpha Manyanga akiwa kwenye mashine ya kuchujia
mafuta kiwanda hapo.
Katika
ushirika wa aina hiyo ni matarajio ya mradi huo kufanikisha juhudi za
kupunguza umaskini kama moja ya malengo ya maendeleo endelevu
yanayotarajiwa na dunia.
Aidha katika upunguzaji huo wa umaskini mradi utachangia ongezeko la fursa za ajira na ukuaji wa uchumi.
Mkoa wa
Dodoma wenye viwanda vya kusindika mbegu za alizeti vinavyofanyakazi
katika mkaazi wakitumia zana dhaifu na vifungashia visivyokuwa na ishara
yoyote ile na kuuza bidhaa zao kando mwa barabara wanahitaji mfumo
thabiti wa ukuzaji wa shughuli zao na kueleweka.
Kutokana na mazingira hayo wajasirimali hawa hujikuta wakiingia hasara kubwa kwa kupoteza tija na pia soko lenye uhakika.
Kutokana
na madhara hayo na pia kukosa hati ya ubora kwa kukosa mazingira
yanayoruhusu hati hiyo kutolewa, TIUMP imelenga kusaidia wasindikaji
hawa na teknolojia sahihi inayohitajika ili watoke pale walipo na kuwa
na viwanda vidogo au vya kati.
Ingawa
kwa sasa UNIDO inasaidia viwanda vinane vya mbegu za alizeti ili kuweza
kuboresha bidhaa zao na utendaji kuna muonekano wa maendeleo makubwa
siku za usoni hasa kwa wanachama wa CEZOSOPA ambao wameuinganishwa
pamoja kwa ajili ya misaada mbalimbali ya kuwawezesha kuwa washindani
katika soko.
Mtaalamu
wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (aliyeipa mgongo kamera) akitoa
maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (kulia)
walipokua wakikagua mtambo wa kusafisha mafuta (Semi re-finery)
uliofadhiliwa na UNIDO kiwandani hapo.
UNIDO
wanatumia maarifa waliyojifunza Ethiopia kuimarisha wanachama wa
CEZOSOPA ambao tayari wamekubali kuunda kampuni ya pamoja na kuwekeza
katika kitu wanachokifanya kwa pamoja kwa lengo la kuongeza uwezo na
ushindani katika soko.
Halmashauri ya Chamwino tayari imekubali kuipa ardhi CEZOSOPA kwa ajili ya uwekezaji huo mkubwa.
Aidha
UNIDO imewezesha kupatikana kwa teknolojia rahisi kwa ajili ya
usafishaji wa mafuta ya alizeti na teknolojia hiyo inafanyiwa kazi na
VETA.
UNIDO
wamesema teknolojia hiyo hiyo inasaidia kuweka mafuta katika viwango
vinavyotakiwa kitaifa na kimataifa na kwamba teknolojia hiyo tayari
inafanyakazi nchini katika viwanda viwili na vingine saba vimeonesha nia
ya kupata teknolojia hiyo.
Imeelezwa kuwa fedha za mradi huo zinapatikana kutoka UNIDO na wadau wengine kama SIDA na UNDAP.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto akipozi kwa picha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akifurahi jambo alipokuwa akipewa
maelezo na Mtaalamu wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (kulia) ya
mtambo mahususi wa kusafisha mafuta (Semi re-finery) uliofahdhiliwa na
UNIDO.
Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga (wa pili kushoto) akimuongoza
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe
wake kukagua mradi huo unaofadhiliwa na UNIDO.
Wakala wa
uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo la Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy akizungumza na
waandishi wa habari nje ya kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha
Glory Farm & Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha
Nzuguni, manispaa ya Dodoma.
Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia) akiendelea kutoa maelezo
ya namna wanavyojaza mafuta yao kwenye vigungashio wakati walipotembelea
na ugeni kutoka Umoja wa Mataifa ulioongozwa na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Pichani
ni madumu yaliyojazwa mafuta ya alizeti kiwandani hapo yakisubiri
kuwekwa nembo maalum na tayari kuingia sokoni kwa mlaji.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akijaza mafuta wakati wa ziara
kwenye kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha cha Glory Farm &
Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya
Dodoma, kinachonufaika na mradi wa ubia wa uboreshaji viwanda kati ya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Wizara ya
Viwanda na Biashara. Kulia ni mfanyakazi wa kiwanda hicho, Mike
Brighton.
Kutoka Dodoma, Tunapeleka malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini kote #HapaKaziTu #GlobalGoals
.....ni maneno ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(wa nne kulia), Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti
cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga
(kulia),Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy (wa
pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa tatu kulia), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika
la UNFPA, Dk. Hashina Begum (wa pili kuhsoto) pamoja na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (wa pili kulia) katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Meneja
Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm &
Agricultural Products, Justin Nyamoga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi
wake wakipozi na bango la kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs).
Afisa
Kilimo wa wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, Aizack Chaula (mwenye suti
nyeusi) akitoa maelezo kwenye shamba la zabibu la heka 300 lililopo
kwenye maandalizi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
aliyeambatana na ujumbe wake kwenye ziara ya kukagua miradi
inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.
Muonekano wa Shamba hilo la heka 300 ikiwa kwenye maandalizi kwa ajili ya kilimo cha Zabibu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na
Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa Zabibu, Sekian Mavunde ili kujua
changamoto zinazowakabili katika kikundi chao. Kushoto ni Mtaalam wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu
Sehemu ya eneo la shamba la heka 296 zilizopandwa Zabibu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitembelea na kupewa maelezo na
Afisa Kilomo wa wilaya ya Chamwino, Aizack Chaula (kulia) kwenye shamba
la Zabibu la Chabuma Amlo’s Ltd. lenye ukubwa wa Heka 296 lililopo
katika kijiji cha Chinangali II, wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambapo
wakulima wa eneo hilo wanaopatiwa msaada chakula kwa vibarua pamoja na
kuchimbiwa mitaro bure shambani hapo na Shirika la Chakula la Umoja wa
Mataifa (WFP). Wengine katika picha ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la
UNFPA, Dk. Hashina Begum ( wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi
wa FAO nchini, Patric Otto (kushoto) waliombatana na Bw. Rodriguez
katika ziara hiyo.
Pichani juu na chini ni miche na vitalu vya Zabibu kabla ya kupelekwa shambani.
Bwawa la umwagiliaji wa kilimo cha Zabibu katika shamba hilo.
Pichani
juu na chini ni wakulima za kilimo cha Zabibu wakizungumzia changamoto
zinazowakabili katika kilimo hicho kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),
Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua miradi
inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na ujumbe wake wakiwa katika
picha ya pamoja na wakulima.
0 comments:
Post a Comment