DR. SHEIN AZURU KIWANDA CHA SUKARI - II



Hili ni jengo la Kiwanda cha Sukari cha Mahonda ambalo linamitambo mbali mbali ambayo inafanyiwa ukarabati wa hali ya juu na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,na baadae mitambo hiyo iweze kuzalisha Sukari itakayouzwa ndani na Nje ya Nchi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinleo alitembelea na kuona hali ya ukarabati huo akiwa katika ziara maalum.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Bw.Rajesh Kumar (katikati) alipotembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,(kulia) Meneja mradi Tushar MEHTA.


Baadhi ya Mashine katika kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiambatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali alitembelea kiwanda hicho leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akionesha kitu wakati alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja leo ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,akiwa katika ziara aliyofuatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali.


Majengo ya Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kiliopo Wilaya ya Kaskazini B.Unguja yakiwa katika hali hiyo inanyoonekana pichani katika ukarabati unaofanywa na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India. Picha na Ikulu.
Source: Michuzi Blog
Share on Google Plus

About Mind 2022

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment