MHESHIMIWA ZITTO AZIDI KUUNGWA MKONO

Elibariki Kingu Emmanuel ni Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi, leo ameibuka kwa mara nyingine tena akibebaa headlines zenye uzito wake baada ya kuthibitisha kukataa posho za vikao vya Bunge.
Mbunge huyo anaanza na haya >>>> Ili niwe na uhalali wa kuikemea Serikali ya chama changu CCM katika matumizi yasiyo ya lazima, lazima nianze na mimi kwa kutochukua fedha zozote za posho (sitting allowance) wakati wote wa Bunge kwa miaka mitano, tayari nimemwandikia Katibu wa Bunge kwamba kwa miaka mitano posho zote ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 200 haitapita kwenye mifuko yangu bali itatumika kwa akina mama wanaoteseka mahospitalini, watoto wanaokosa madawati na kuboresha miundombinu“- Mbunge Elibariki Kingu
Hajaishia hapo, anaendelea hivi kwenye sentensi nyingine >>> “Kwa dhamira safi tukiamua kubana posho mimi na Wabunge wenzangu tutafika mbali, na ninaomba wabunge wenzangu wanisapoti.. nimeona sina sababu ya kuchukua pesa kwa sababu ninalipwa mshahara… sitakuwa wa kwanza kupinga uchukuaji wa posho kwa kuwa kuna watu tayari walianza kuonyesha pia nia hiyo akiwemo Zitto Kabwe, ninaamini wabunge wataonyesha uzalendo“– Elibariki Kingu.
Kama jambo hili la kukataa posho kwa wabunge litatekelezwa kwa wote ni dhahiri tungefika mbali kwa kuwa fedha hizi zingefanya kazi kubwa… Bunge lina jumla ya wabunge 394, vikao vya Bunge kisheria kwa mwaka ni wastani wa vikao 140 mpaka 180, sasa kila mbunge akilipwa 220,000 kila siku kwa wabunge 394, ukipiga hesabu kwa miaka mitano utaona ni kiasi gani cha pesa kitaokolewa” >>> Elibariki Kingu.
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment