Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015
Na RFI
Mauricio
Macri kutoka chama cha Kiliberali amechaguliwa Jumapili hii kuwa rais wa
Argentina katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. uchaguzi ambao
umeashiria mwisho wa utawala wa Kirchner alieliongoza taifa hilo la tatu
kwa uchumi katika eneo la Amerika ya Kusini.
Tafiti
angalau nne wa ziliofanywa na televisheni baada ya uchaguzi, zinampa
ushindi Meya wa Buenos Aires. Matokeo ya kwanza rasmi yalikua
yanatarajiwa kutangazwa saa 1:30 usiku saa za Argentina (sawa na 4:30
usiku saa za kimataifa).
Mauricio
Macri, mwenye umri wa miaka 56, amemshinda Daniel Scioli, mgombea wa
serikali ya mseto, ambaye alikuwa alipewa nafasi kubwa ya kushinda kabla
ya duru ya kwanza ya uchaguzi.
Daniel Scioli akipiga kura katika kata ya Tigre, katika jimbo la Buenos Aires Novemba 22, 2015.
Rais
Cristina Fernández de Kirchner kutoka chama cha mrengo wa kushoto,
anaiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2007 baada ya kumrudilia mume wake,
ambaye hakuweza kugombea awamu ya tatu mfululizo, kwa mujibu wa katiba.
Mara tu
baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza, wafuasi wa meya wa Buenos
Aires, walikutana katika makao makuu ya muungano wa vyama vya upinzani
wa Cambiemos (ikimaanisha tubadili) unaongozwa na Macri, wamejipongeza
na kuanza kusherehekea ushindi.
Wafuasi wa Mauricio Macri jijini Buenos Aires, Novemba 22, 2015.
Mauricio
Macri atajitahidi kushirikiana na taasisi zingine za uongozi wa nchi
kwa kuliongoza taifa hilo, kwani muungano wake hauna wingi wa viti
katika Baraza la wawakili na Baraza la Seneti.(P.T)
0 comments:
Post a Comment