By Lilian Lucas, Mwananchi Digital
Morogoro. Nyati tisa wa hifadhi ya taifa ya Mikumi wamegongwa na kufa papo hapo wakati wakivuka barabra ya Morogoro-Iringa na gari aina ya fuso iliyokuwa ikitokea Ifakara kwenda Chalinze. Akizungunza na Mwananchi Digital leo, mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo ya taifa iliyopo mkoani Morogoro, Dattomax Sellanyika amesema wanyama hao wamegongwa jana usiku katikati ya hifadhi hiyo na dereva wa lori hilo anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi.
Amesema kuwa licha ya kuwepo alama ndani ya hifadhi zinazotoa mwongozo wa mwendokasi, dereva huyo alikaidi na hatimaye kuisababishia hasara kubwa hifadhi hiyo. Ameuomba uongozi wa mkoa wa Morogoro kuharakisha ujenzi Wa barabara ambayo ilikubaliana kujengwa nje ya hifadhi kwa leongo la kuepusha ajali dhidi ya wanyama ndani ya hifadhi ya Mikumi.
Source: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment