MAWAZIRI WATUMA SALAMU KWA WATENDAJI

MAWAZIRI na Naibu mawaziri walioteuliwa wiki hii, wameapishwa jana na kuanza kazi kwa kutoa matamko kwa watendaji, kuendana na kasi na Rais John Magufuli. Moja ya matamko hayo, limetumwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya, ambao wamepewa miezi sita kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayekaa chini shuleni.
Lingine limetumwa kwa waliokiuka sheria na kujenga kwenye maeneo ya wazi na katika fukwe za bahari, ambako wametakiwa kuondoka bila kusubiri nguvu mpya iliyopo sasa.
Simbachawene, wanaokaa chini Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene aliwataka watendaji katika halmashauri ambao hawawezi kwenda na kasi yake, wajiandae kuondoka.
Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya, kuacha kazi ya kupokea viongozi wanaoingia katika maeneo yao, bali wafanye kazi kwenda na kasi yake ili kuhakikisha miezi sita kuanzia Januari mwakani, kusiwe na mwanafunzi anayekaa chini.
“Ni lazima wafanyekazi kwa kubadili maisha ya Watanzania hivyo ni lazima baada ya miezi sita, kusiwe na mtoto anayekaa chini na anayeona hawezi ni vyema apishe wanaoweza waendelee,” alisisitiza.
Aliwataka Watanzania kutarajia matokeo makubwa katika wizara hiyo hasa Tamisemi, kwani inagusa masuala makubwa ya wananchi. Lukuvi na bomoa bomoa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema atatekeleza kwa uwezo wake malengo ya Rais John Magufuli na Ilani ya chama na kwake itakuwa kazi tu.
Alisema nia yake ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya kumilikishwa ardhi kisheria na wanakuwa sawa katika ardhi na kuendelea na spidi ya kutetea wanyonge, ili waache kunyanyaswa katika masuala ya ardhi.
Alitoa tahadhari kwa waliokiuka sheria kwa kujenga katika maeneo ya wazi au fukwe, wajiandae kuondoka wenyewe, wasisubiri nguvu zake kwani sasa amekuja na nguvu mpya.
“Natarajia kutumia utaratibu mpya wa kutoa namba za simu ili kila Mtanzania mwenye shida au anayetaka kumfikia waziri kuzungumzia malalamiko ya ardhi, anafanikiwa,” alisema.
Alisema katika utaratibu huo wa kutoa namba maalumu ya simu, wote walioonewa na watu wanaojifanya wenye fedha kwa kuwapora ardhi masikini, watatakiwa kutoa malalamiko yao na kumfikia kwa urahisi.
Ummy, Kigwangala Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, yeye alisema atahakikisha changamoto zote katika sekta ya afya, zinafanyiwa kazi ikiwemo upatikanaji wa dawa na wataalamu.
Alisema atahakikisha wanapatikana wataalamu wa kutosha na kuongeza uwezo wao, huku akitaka wananchi kumpa ushirikiano kwa kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji na ufanisi. Katika masuala ya jinsia, alisema atahakikisha sheria zote kandamizi kwa wanawake na watoto zilizolalamikiwa na makundi mbalimbali kwa muda mrefu, zinafanyiwa kazi. Mwalimu aliungwa mkono na Naibu wake, Dk Hamis Kigwangala, aliyesema atafanya kazi kwa kasi hivyo wananchi watarajie mabadiliko katika sekta hiyo.
Bima kwa wote Alitaja mambo watakayohakikisha yanafanyiwa kazi kuwa ni kila Mtanzania awe na bima ya afya, kujenga kituo cha afya katika kila kata, kila kijiji kuwa na zahanati, upatikanaji wa dawa kwa bei nafuu katika hospitali za Serikali, vifaa tiba, vitenganishi na vifaa vya kutosha. Pia alisema watumishi wa sekta ya afya watapata motisha ya kufanya kazi, ili wawahudumie vizuri Watanzania na kuondoa malalamiko kwa wananchi. Dk Mwakyembe.
Habari Leo
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment