Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubana matumizi yasiyo ya lazima ambapo imetangaza kufuta posho za vikao vya bodi vya Bunge.
Akitangaza uamuzi huo jana Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru alisema kuwa serikali imefuta posho hizo kwa kuwa wabunge hulipwa na Bunge. Alisema kuwalipa posho ya vikao vya bodi ni kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja (double invoicing).
“Mtu mwingine anakuwa kwenye bodi zaidi ya moja kwa sababu anajua kuwa kuna posho, hii haikubaliki,” alisema Mafuru.
Katika hatua nyingine, Mafuru ameeleza kuwa vikao vya bodi za mashirika ya umma hivi sasa vitakuwa vikao vinne tu kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment