UKAWA WAITIKISA CCM ARUSHA MJINI



*Matokeo ya awali, Lema aelekea kushinda ubunge

*CCM, CUF waumana Handeni Mjini, Wachachewajitokeza
NA WAANDISHI WETU, ARUSHA/TANGA
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema, anaelekea kurejea tena bungeni  huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake, Philemon Mollel wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika matokeo ya awali ambayo yalibandikwa vituoni katika baadhi ya kata za Arusha, yanaonesha  Lema anaongoza takribani katika vituo vyote, jambo ambalo ni dalili za kuibuka kuwa mshindi wa nafasi hiyo ambayo anaitetea kwa kipindi cha pili.
Pamoja na idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza katika uchaguzi huo  tofauti na uchaguzi uliopita, haikumzuia Lema kuongoza katika matokeo hayo ya awali ambayo yalibandikwa vituoni.
Matokeo hayo ya awali yanadhihirisha mwitikio wa wapiga kura wa Arusha dhidi ya kauli iliyotolewa juzi na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyewataka wananchi wa jimbo hilo kupiga kura  kwa wingi.
Katika matokeo hayo ya awali Kata ya Daraja Mbili Chadema ilikuwa imekwisha jihakikishia ushindi katika kata hiyo kwa kuibuka na kura 1,572 huku CCM ikiambulia kura 916.
Katika vituo vingine matokeo yalikuwa kama ifuatavyo. Kata ya Elerai Kituo cha Shule ya Msingi Mama Mussa, kituo namba 1, CCM 69, Chadema 70, Mama Musa namba 2, CCM 63 na Chadema 67, kituo cha Remtula namba 1 Chadema 56 na CCM 50, Remtula 2 Chadema kura 54 na CCM kura 35, kituo cha Remtula namba 3 Chadema kura 68, CCM 66 na ACT kura 1 namba 4. Chadema kura 46 na CCM kura 43
Kituo cha shule ya Msingi Elerai Majengo kituo namba 2 Chadema 67, CCM 62, CUF 1, Majengo A  Chadema kura 94, CCM kura 29, Majengo A1 Chadema kura 106 na CCM kura 34.
Mtaa wa Olkereyan Kata ya Olasiti kituo namba 2, waliopiga kura walikuwa ni 151 ambapo Chadema ilipata kura 109, CCM kura 40,  ACT kura 1 huku kura moja ikiharibika.
Katika Kata ya Levolosi, Shule ya Msingi Levolosi kituo namba 2 Chadema kura 100, CCM kura 48, ACT kura 0, CUF kura 0 na NRA kura 0.
Kata ya Olasiti Kituo cha Shule ya Msingi Olasiti kulikuwa na vituo saba ambapo kituo cha kwanza Chadema kura 107, CCM kura 75 na ACT kura 1.
Kituo cha Pili Chadema kura 112, CCM kura 77, kituo namba tatu Chadema kura 111, CCM kura 58. Kituo namba 4 ChademaA kura 102, CCM kura 87, kituo namba 5 Chadema kura 78,  CCM kura 102,  ACT kura 1, kituo namba 6 Chadema kura 113, CCM kura 91, ACT 2, na kituo namba 7 Chadema kura 81, CCM 73 na ACT kura 2.
Kituo cha Osunyai kulikuwa na vituo vitano ambapo kituo cha 1 Chadema kura 123, CCM kura 59,  kituo cha 2, Chadema kura 110, CCM kura 64, kituo cha 3, Chadema kura 129, CCM kura 41, kituo cha  5, Chadema kura 103 CCM kura 50 na kituo cha  6 Chadema .kura 103 na CCM kura 49. Kituo cha 7, Chadema kura 109 na CCM kura 44.
Katika Kituo cha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kata ya Sekei mgombea wa Chadema aliibuka katika vituo vyote vitatu ambapo kituo cha kwanza Chadema ilipata kura 115 na CCM kura 50, kituo cha pili Chadema  kura 67 na CCM 61, kituo cha tatu Chadema 76 na CCM kura 57.
Wasimamizi na WhatsApp
Katika hali ambayo haikutarajiwa baadhi ya wasimamizi na mawakala wa vyama vya siasa katika Jimbo la Arusha Mjini walijikuta wakitumia muda mwingi kuchati na simu  ikiwamo kutumia mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’  kutokana na idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza katika vituo 721.
Pamoja na hali hiyo wengine walijikuta wakiwa wamepumzika kwenye viti, huku wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubiri wapiga kura.
Moja ya sababu  iliyosababisha kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura vituoni, ni kuwapo kwa dalili ya mvua kubwa  ambayo iliambatana na wingu zito kutanda kuanzia saa 4 asubuhi na ilipofika saa 9 alasiri mvua ilianza kunyesha.
Kutokana na hali hiyo watu wengi walijifungia ndani ya nyumba zao na wengine walikuwa katika nyumba za Ibada au kumbi za starehe na kuupa kisogo uchaguzi huo.
Handeni Mjini
Taarifa kutoka wilayani Handeni, zilizopatikana jana jioni wakati tukienda mtamboni, zilieleza kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Omari Kigoda, alikuwa akiongoza katika matokeo ya awali dhidi ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Remmy Shundi.
Katika matokeo hayo ya awali yanaonesha katika Kata ya Chanika, CCM ilikuwa ikiongoza kwa kupata kura 1,275, CUF 275, Chadema 57 na ADC 36.
Kata ya Mabanda, CCM 783, CUF 541, Chadema 27, ADC 66 na TLP kura tatu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa kata alisema kitendo cha kukatika kwa umeme kimesababisha kuchelewa kwa matokeo katika baadhi ya kata.
Mtanzania
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment