NAULI ZA MABASI YA DART KUJADILIWA KESHOKUTWA

Kituo cha mabasi yaendayo kasi cha Kimara

Kituo cha mabasi yaendayo kasi cha Kimara Baruti, Dar es Salaam kama kilivyokutwa jana kikiwa kimeharibiwa na wananodaiwa kuwa ni madereva wa mabasi hayo. Picha na Salim Shao 
By Jackline Masinde
Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeandaa mkutano wa kujadili viwango vya nauli za mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri wa haraka jijini hapa, keshokutwa.
Mapendekezo ya nauli zilizowasilisha na Kampuni ya Uda Rapid Transit (UDA-RT) zitakazojadiliwa ni Sh700, Sh1,200 na Sh1,400.
Mapendekezo ya nauli hizo ni kwa watu wazima, lakini iwapo yatapita wanafunzi watalipa nusu yake kwa kila safari.
Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo, David Mziray alisema mkutano huo una lengo la kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau na watumiaji wa usafiri nchini.
“Mamlaka imelazimika kuandaa mkutano utakaofanyika Jumanne ya wiki inayokuja utakaowahusisha wananchi wote kujadili kama nauli hizo zinafaa au zinahitaji marekebisho,” alisema.
Mziray alisema huo ni utaratibu wa Sumatra kisheria kabla hawajafanya uamuzi wa kupitisha nauli huwashirikisha wananchi kutoa maoni yao.
“Maoni yatakayotolewa na wananchi pamoja na wadau yatatusaidia kubaini upungufu uliopo katika nauli hizo na kuurekebisha, lakini pia hayawezi kuwa ndiyo uamuzi wa mwisho,” alisema.
Alisema kuwa baada ya wananchi kutoa maoni yao, Sumatra itakaa na kutoa uamuzi.
Akizumgumzia kucheleweshwa kwa ukusanyaji wa maoni hayo, alisema kampuni inayotaka kutoa huduma hiyo ilichelewa kuwasilisha mapendekezo yake.
“Haya mapendekezo yalitufikia siku ya Jumatano ya wiki hii, baada ya kampuni hiyo kuyaleta kwa mara ya kwanza, lakini yakashindwa kupokelewa na Sumatra kutokana na kukosa baadhi ya vielelezo, alisema Mziray.
Mkurugenzi wa Uda Rapid Transit, Sabri Mabruk alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa mapendekezo ya nauli hizo alisema zipo sababu nyingi, lakini alikataa kuzitolea maelezo kwa madai kuwa yupo kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka na kumtaka mwandishi ahudhurie mkutano huo.
Mwananchi
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment