POLISI YAWASAKA WAHARIRI MAWIO

Polisi yawasaka wahariri Mawio.

Picha ya maktaba ikimwonyesha Mkurugenzi wa
Picha ya maktaba ikimwonyesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene akiwa ameshika gazeti la Mawio Aprili 22, 2014 alipokutana na wanahabari baada ya gazeti hilo kuandika habari kuhusu hati ya Muungano. 
By Kalunde Jamal, Mwananchi
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawasaka wahariri na mmiliki wa gazeti la Mawio kutokana na habari mbalimbali ambazo wamekuwa wakichapisha.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema jana kuwa wahariri hao wanatafutwa kwa ajili ya kusaidia uchunguzi unaofanyika kuhusu habari walizokuwa wakiziandika.
Sirro alisema wamekuwa wakiandika na kuchapisha habari ambazo zina utata, hivyo wanatafutwa kwa ajili ya kuthibitisha ukweli wake.alisema Siro.
Mbali na kusakwa kwa wahariri hao, jana kwenye mitandao ya kijamii, ilisambaa taarifa iliyoonekana kama tangazo la Serikali ya kulifungia maisha gazeti hilo bila kueleza sababu za hatua hiyo, ingawa halikuwa na saini ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye aliyetajwa kuandaa tangazo hilo.Nape alipotafutwa na Mwananchi kwa simu kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa ujumbe mfupi, “samahani, nipo kikaoni tuma msg!” Hata alipotumiwa ujumbe huo hakujibu.
Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyepatikana jana kuzunguzia taarifa hiyo.
Hata hivyo, baadaye usiku, Idara ya Habari (Maelezo), ilitoa taarifa kuwa Waziri Nape atazungumza na waandishi wa habari leo saa sita mchana, lakini haikueleza katika mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa idara hiyo atazungumzia nini.
Kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, Waziri wa Habari anaweza kulifungia gazeti wakati wowote akijiridhisha kwamba halikuendana na masilahi ya umma. Sheria hiyo imekuwa ikipingwa kwa maelezo kuwa imepitwa na wakati na inakandamiza uhuru wa habari     
Mwananchi
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment