MAGUFULI AAGIZA FEDHA ZA SHEREHE ZA UHURU ZIJENGE BARABARA, PROF. LIPUMBA AMTEMBELEA



RAIS Dkt. John Pombe Magufuli, ameamuru fedha zilizotengwa ili kugharamia shamrashamra za Sherehe za Uhuru Desemba 9, mwaka huu, zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Mwenge hadi Morocco, Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 4.3.

Alisema fedha hizo pia zitatumika kuongeza njia mbili za barabara kwa kiwango cha lami na tayari kiasi cha sh. bilioni 4, zimeamriwa zipelekwe kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) ambapo agizo hilo linapaswa kuanza mara moja.


Rais Dkt. Magufuli aliyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na kusisitiza kuwa, anataka kuona ujenzi wa barabara hizo unaanza haraka ili kukabiliana na msongamano wa magari.

Alisema kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morocco hadi Mwenge kuwa na njia tano ambazo zitapunguza tatizo la foleni jijini Dar es Salaam kwani hivi sasa kuna kero kubwa.


Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli amekutana, kufanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Ikulu, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, Prof. Lipumba alimpongeza Rais Dkt.Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano na kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11.


Kwa upande wake, Rais Dkt. Magufuli alimpongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga vitendo vya kifisadi na kumtakia heri katika shughuli zake. 

Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment