KUBENEA AMPELEKA SPIKA WA BUNGE MAHAKAMANI


Spika wa Bunge la 11, Job Ndugai
Spika wa Bunge la 11, Job Ndugai
MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea amesena anatarajia kwenda Mahakama Kuu kwa ajili ya kuomba tafsiri ya vifungu vya sheria kutokana na Spika wa Bunge, Job Nduga kuwaruhusu askari wa uraiani kuingia ndani ya bunge na kuwatoa nje wabunge kambi rasmi ya Upinzani. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Wabunge hao walitolewa nje baada wa kupinga uwepo wa Dk Ally Mohamed Shein kwa kile walichodai si Rais halali wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Kubenea amesema kwa mujibu wa katiba na sheria za bunge ukomo wa Rais na wabunge ni miaka mitano hivyo ukomo wa Dk Shein ilikwa ni Novemba 2 mwaka huu hivyo angepaswa kuingia bungeni kama mgeni mualikwa.
Amesema kuwa sheria za bunge haziruhusu mtu kuingia ndani ya ukumbi zaidi wa wabunge na mpambe wa bunge hivyo Spika alifanya makusudi kuwaruhusu , jeshi la polisi, jeshi la wananchi, Spika la baraza la wawakilishi Zanzibar na makamu wa pili wa rais Zanzibar.
“Mimi sitaruhusu kanuni na taratibu za bunge zivunje ili hali nikiwa ndani ya bunge na ndio maana nimepanga kunda mahakamani ndani ya wiki hii kumshitaki Ndugai kwa kuvunja kanuni hizo,” amesema.
“Tulipata taarifa kuwa Serikali ya John Magufuli wamepanga njama za kutudhuru sisi wabunge wa upinzani na kutokana na vitenda hivyo nimewasiliana na wakili wangu Peter Kibala ili kuweza kumburuza Ndugai kwenda mahakani,” aliongeza Kubenea.
Kambi ya Upinzani haiwezi kukubali kutawaliwa kibabe na Ndugai akiendelea kuendesha bunge kibabu litamshinda na wao wataendelea kupayuka.
Aliendelea kusema kuwa katika mkutano wa kwanza wa bunge la 11 inadhihirisha wazi kuwa Ndugai si kiongozi bora na kama taratibu nyingine zingufuatwa asingepa nafasi hiyo.
Kwa upande mwingine Kubenea ametaka manispaa ya Kinondoni kusitisha mara moja zoezi la bomoabomoa lililoanza hivi karibuni kwani linafanywa kinyume cha sheria.
Alisema kitu cha msingi ni kufuata sheria ili watakaobomolewa nyumba zao wasiende mahakani kudai fidia.
“Sheria zisipofuatwa ni wazi kuwa watakaobomolewa nyumba zao watakapoenda mahakani kudai fidia na wakishinda halmashauri italazimika kulipa fidia, lakini pia ikumbukwe halmashauri hiyo itakuwa chini ya upinzani hivyo hatutakubali kulipa fidia hizo,” amesema Kubenea.
chanzo:mwanahalisionline
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment