Chama
cha mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa ubunge Jimbo
la Ulanga baada ya mgombea wake, Goodluck Mlinga kupata kura 25,902 sawa
na asilimia 69.78 akiwashinda wapinzani wake katika uchaguzi
uliofanyika jana wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya
Ulanga usiku wa kuamkia leo, Isabela Chilumba alimtangaza mgombea wa
CCM, Goodluck Mlinga kuwa ndiye mshindi wa kiti hicho baada ya kuwabwaga
wenzake wa chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) na ACT-Wazalendo.
Mgombea
wa CHADEMA Pancras Michael Ikongoli alipata kura 10,592 sawa na
asilimia 28.53 wakati mgombea kupitia ACT-Wazalendo yeye akipata kura
6,26 sawa na asilimia 1.69
Uchaguzi
huo umefanyika Novemba 22 ikijumuisha vituo vya kupigia kura 203 katika
kata 21 huku kukiwa na idadi ya wapigakura 76,715 waliojiandikisha
katika daftari la kudumu la wapigakura.
Jumla ya wapigakura 37,499 walijitokeza kupiga kura huku kura 379 zikiharibika wakati kura halali zikiwa 37,120.
Kwa
upande wa mgombea wa CCM, Goodluck Mlinga aliwashukuru wananchi wa
jimbo la Ulanga kwa kumchagua kuwa mbunge wao na kuahidi kuitumikia kazi
hiyo kwa moyo mmoja na kuomba ushirikiano kutoka kada mbalimbali ili
kutekeleza majukumu yake hayo mapya.
0 comments:
Post a Comment