LOWASSA, MBOWE, SUMAYE WAFIKA MAHALI ALIPOUAWA MAWAZO

BY DANIEL MKATE


Marehemu Alphonce Mawazo
Wakati mwili wa marehemu Alphonce Mawazo, ukitarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Chikobe, wilayani Geita, aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Ukawa, Edward Lowassa, amewaongoza viongozi waandamizi wa chama hicho eneo alilouawa mwenyekiti huyo wa Chadema mkoani humo.
Msafara wa Lowassa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, wakiwa na wabunge zaidi ya 50 na wanachama na wafuasi wa chama hicho, walienda eneo hilo lililopo  jirani na makazi ya watu na kujioneo hali halisi.
Baada ya kufika eneo hilo alilouawa Mawazo, viongozi hao walisimika  bendera ya chama hicho pamoja na kuzungusha utepe mwekundu kuashiria sehemu iliyomwagika damu.
Baadhi ya watu baada ya kuliona eneo hilo walibubujikwa machozi, huku wakiamini kifo hicho kilipangwa kutokana na kushambuliwa eneo la wazi katika barabara kuu ya Geita - Katoro.
LOWASSA AMPONGEZA JAJI
Lowassa akizungumazana na waombolezaji katika viwanja vya Mnadani mjini Katoro, alimpongeza Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kwa kutoa uamuzi wa haki dhidi ya polisi waliozuia kuagwa kwa mwili wa Mawazo jijini Mwanza.
Alisema uamuzi wa Jaji Mlacha unatakiwa kusambazwa nchi nzima iwe fundisho kwa Jeshi la Polisi nchini.
"Polisi hawafahamu haki za wananchi lakini Jaji Mlacha amewafundisha na kutakiwa kuacha mchezo na maisha ya watu," alisema.
HUKUMU KUWEKWA MAGAZETINI
Lowassa alisema hukumu hiyo itawekwa katika magazeti mbalimbali ili iweze kusomwa na polisi pamoja na wanaodhulumiwa haki zao.
Alirejea kauli yake ya kuwataka polisi kuwakamata wote waliohusika na mauaji ya Mawazo la sivyo watashagulika wenyewe. Hata hivyo, hakusema watashughulika kwa namna gani.
SUMAYE
Naye Sumaye aliwataka wanachma wa Chadema watulie kipindi hiki bila kuchukua maamuzi magumu wakati wanaendelea  na msiba wa Mawazo.
"Tulikuja uwanja huu kuomba kura tukiwa na Mawazo, lakini Leo (jana) tumekuja naye akiwa mfu, tumempoteza kamanda wetu," alisema Sumaye.
MBOWE
Mbowe alisema hawatamsahau Mawazo kutokana na kujitoa kwake katika chama.
"Ukimtuma aende Sumbawanga hata kama hana nauli, alidandia hata Fuso na kisha pesa anatumiwa akiwa njiani," alisema Mbowe.
MWILI WAAGWA GEITA
Mwili wa Mawazo jana uliagwa mkoani Geita katika viwanja vya Magereza kisha Katoro Jimbo la Busanda alilowania ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu na kushindwa.
Aliuawa Novemba 14, mwaka huu na watu wasiojulikana katika mji wa Katoro.
SOURCE: NIPASHE
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment