MATATIZO YA WANAWAKE KUTOPATA UJAUZITO HARAKA (INFERTILITY) - 2

preg
Wiki hii nitamalizia mada hii niliyoianza wiki iliyopita. Matatizo mengine yanayomfanya mwanamke asipate ujauzito anapohitaji ni kutokufahamu siku za kupata mimba. Ili kufahamu siku za kupata mimba lazima ufahamu kwanza mzunguko wako uko vipi, mada hii tutakuja kuiongelea katika makala zijazo.

Vilevile mwanamke ajue siku zake za ute wa uzazi. Ute wa uzazi upo wa aina tatu, kuna mwepesi, mwepesi na kuvutika na mzito.
Ute wa uzazi ndiyo unaokuwezesha upate ujauzito. Suala la kufahamu mzunguko wa hedhi, siku za kupata mimba ni suala linalowahusu wote wawili, mume na mke.
Matatizo ya kisaikolojia kwa mwanaume na mwanamke, unene kupita kiasi huchangia tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO
Kama tulivyoona, kitendo cha mwanamke na mumewe kukaa zaidi ya mwaka wanatafuta mtoto ni tatizo kwa hiyo linahitaji uchunguzi ambao  unafanyika pande zote mbili.
Mwanamke anayesumbuliwa na maumivu chini ya tumbo mara kwa mara naye yupo katika hatari hii kwani upo uwezekano wa kuathiri mirija yake ya uzazi na ikaziba kabisa, mzunguko wa hedhi unavurugika na kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Wanawake wengine hupata maumivu ya kiuno na tumbo kwa muda mrefu, siyo dalili nzuri. Matiti au chuchu kutoa maziwa pia huathiri kwa kiasi kikubwa.
Maumivu wakati wa hedhi pia si dalili njema katika mfumo wa uzazi kwani inaweza kuwa una maambukizi sugu ya kizazi, uvimbe katika kizazi au tabaka la ndani la kizazi kuwa nje. Hizi ni dalili chache kwa mwanamke.
Kwa upande wa mwanaume dalili pia zipo nyingi lakini kama nilivyoelezea hapo awali, ila kama mwanaume anashindwa kufanya tendo la ndoa hilo ni tatizo kubwa, maumivu ya njia ya mkojo, maumivu ya korodani, kutotoa kabisa manii pia ni mojawapo ya tatizo.
Mwanaume anaweza kupata matatizo ya uzazi endapo atavuta sana sigara na matumizi ya vilevi kwa muda mrefu hasa pombe kali na madawa ya kulevya.

UCHUNGUZI
Hufanyika katika kliniki za magonjwa ya akina mama kwenye hospitali za mikoa na rufaa.
 Muone daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na uzazi katika hospitali hizo akuchunguze.
Epuka matumizi ya dawa bila ya kufanyiwa uchunguzi hospitali. Vipimo mbalimbali  hufanyika kama vipimo vya damu kuangalia homoni na maambukizi mengine yanayokwamisha vipimo vya ‘Ultrasound’, mirija kiitwacho HSG na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa. Mwanaume atapimwa mbegu za uzazi.

USAHURI NA TIBA
Wahi hospitali ya mkoa au wilaya kwa uchunguzi. Zingatia maelekezo ya daktari wako ili uweze kufanikiwa.

Share on Google Plus

About Mind 2022

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment