Wachezaji watano wanawania tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa 2015.
Wachezaji hao ni:
1. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon na Borussia Dortmund (Ujerumani)
2. André Ayew - Ghana na Swansea City (Uingereza)
3. Yacine Brahimi - Algeria na FC Porto (Ureno)
4. Sadio Mané - Senegal na Southampton (Uingereza)
5. Yaya Touré - Ivory Coast na Manchester City (Uingereza)
Mshindi ataamuliwa na mashabiki wa soka Afrika ambao wamepewa fursa kupiga kura hadi saa 1800 GMT tarehe 30, Novemba.
Unaweza pia kupiga kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa nambari +44 7786 20 20 08:
- Ujumbe 1 kwa-Emerick Aubameyang
- Ujumbe 2 kwa André Ayew
- Ujumbe 3 kwa Yacine Brahimi
- Ujumbe 4 kwa Sadio Mané
- Ujumbe 5 kwa Yaya Touré
Ada za matumizi ya simu za kimataifa zitatozwa.
Tafadhali wasiliana na mtoaji huduma wako kwa maelezo zaidi. Kumbuka, ni ujumbe moja utatumika kwa nambari moja ya simu pekee.
Mshindi atatangazwa Ijumaa tarehe 11 mwezi Decemba wakati wa matangazo maalum kwenye BBC World News na BBC World Service saa 1530-1600 GMT, na tangazo pia litatolewa katika mitandao ya BBC Sport na BBC Africa. Unaweza ukashiriki mjadala huu kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia #BBCAFOTY Kwa sheria na masharti bofya hapa.
Wagombea wa tatu mwaka huu waliopigiwa kura na wanahabari 46 kutoka Afrika wamewahi kushinda tuzo hilo: Ayew (2011), Touré (2013) na Brahimi (2014).
Aubameyang ameorodheshwa kwa mwaka wa tatu mfululizo wakati Manéakijumuishwa kwa mara ya kwanza.
Walioshinda Tuzo ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka kwa miaka iliyotangulia ni:
Yacine Brahimi (2014);
Yaya Touré (2013);
Christopher Katongo (2012);
André Ayew (2011);
Asamoah Gyan (2010).
0 comments:
Post a Comment