Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji amesema kampuni yake inaongoza sekta binafsi kwa kutoa ajira kwa vijana.
Kampuni hiyo pia inamiliki mashamba makubwa ya mkonge yaliyopo katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Kilimanajaro.
Dewji alisema kuwa ana kampuni 31 ambazo zinatengeneza bidhaa mbalimbali za Kitanzania ambazo zinatoa fursa ya ajira kwa vijana wengi.
Alisema hayo baada ya kutwaa tuzo ya ‘Person of The Year’ iliyotolewa na jarida maarufu duniani la Forbes, huku akibainisha kuwa tuzo hiyo inaashiria namna utajiri wake umekuwa kwa kasi kubwa katika kipindi kifupi.
Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kupokea tuzo hiyo, alisema mafanikio yake yametokana na matumizi ya teknolojia ya juu inayomsaidia kuendana na ushindani unaobadilika kila siku.
“Heshima hii haitokani na utajiri nilionao, bali ni ubora wa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni zangu kugusa maisha ya watu wa aina zote,” alisema Dewji na kuongeza:
“Nina viwanda 31 ambavyo vimekuwa vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na kuziuza kwa Watanzania kwa gharama nafuu ya kuanzia dola 200. Pia, Ulaya nina kiwanda cha kanga na vitenge ambacho malighafi zake zote zinatoka Tanzania naingizia Serikali kipato kwa kulipa kodi ipasavyo,” alisema.
Alisema alipata maono ya utajiri wake hasa kutoka kwa baba yake, Ghulam Dewji na kumwita mjasiriamali shujaa ambaye alianzia kwenye udereva wa malori hadi kufikia kuwa milionea. Alisema baba yake alimshirikisha katika biashara tangu akiwa mdogo.
0 comments:
Post a Comment