1448618511-hellen (1)
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36),  aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi – Shughuli za Bunge, (Pichani) kilichotokea ghafla mapema Ijumaa ya Novemba 27.2015, wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Msiba upo nyumbani kwake eneo la Kisasa, Mjini Dodoma. Taarifa zaidi na taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na ratiba kamili ya maziko zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu pindi mipango itakapokamilika.
BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
27.11.2015.