Ulaji wa Miraa unaathiri
nguvu za kiume.
Utafiti uliofanywa kwa
niaba ya serikali ya Kenya na wahadhiri wa chuo kikuu cha Moi kilichoko katika
Bonde la ufa umebaini kuwa Majani ya miraa inayofahamika pia kama 'Mairungi'
unazuia ukuaji wa manii.
Aidha ulaji wa kipindi
kirefu wa miraa unafanya mbegu za kiume za wanaume kufa haraka pindi
zinapowekwa kwenye uke.
Mtafiti mkuu wa chuo
kikuu cha Moi, Ochiba Lukanda, anasema kuwa utafiti sawa na huo uliofanywa huko
ghuba ulibaini matokeo kama hayo.
Lukanda anasema kuwa
wanaume ambao wamekuwa wakila Miraa kwa kipindi kirefu na wakaacha huwa
wanapata uwezo wao wa kutunga mimba.
Ulaji wa Miraa pia
huwa unasababisha mshtuko wa moyo.
''Mtu anapokula mmea
huu baada ya muda damu yake huaanza kwenda kwa kasi, mbali na shinikizo la damu
mumea huu hausababishi saratani kama inavyodaiwa '' Dakta Lukanda
Hata hivyo utafiti
katika maeneo yanayokuzwa mumea huu umetambua kuwa idadi ya vijana wanaokataa
kwenda shule kwa sababu ya kujishughulisha na uchumaji wa Miraa na upakiaji wa
matawi yake.
''kutokana na utashi
wa bidhaa hiyo,malipo ya wafanyikazi wanaoishughulikia ni ya juu mno kwa hivyo
inawavutia vijana kuacha masomo alisema daktari huyo.
Daktari Lukoye Atwoli
alisema kuwa miraa husababisha walaji wake kuwa na mori na hata wakati mwengine
msongo wa mawazo.
Utafiti huu unafwatia
ule uliofanywa mwaka uliopita na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Nairobi kwa
ushirikiano na chuo kikuu cha Konstanz cha Germany na kile cha Minnesota,
Marekani uliobaini kuwa ulaji wa miraa unaathiri ubongo wa walaji wake na
kusababisha msongo wa mawazo,mafadhaiko na mahangaiko ya kiakili mbali na
matatizo mengine chungu nzima.
0 comments:
Post a Comment