UTURUKI KUREJESHA MWILI WA RUBANI WA URUSI

Rubani huyo alipigwa risasi na wapiganaji wa Syria baada ya kutumia mwamvuli kuchupa kutoka kwenye ndege, baada ya ndege hiyo kupigwa kombora na Uturuki.
Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Uturuki , Ahmet Davutoglu, mwili wa luteni kanali Oleg Peshkov utakabidhiwa serikali ya Urusi.
Bwana Davutoglu amesema kuwa waasi wa jamii ya Turkmen wanaoishi kwenye mpaka wa Syria na Uturuki walimpiga risasi marehemu luteni kanali Peshkov aliporuka kwa mwavuli baada ya ndege yake kudunguliwa.



Image copyright
Image captionWaasi hao wanaoungwa mkono na Uturuki wanasema kuwa alikuwa amekata roho alipofika ardhini.

Waasi hao wanaoungwa mkono na Uturuki wanasema kuwa alikuwa amekata roho alipofika ardhini.
Davutoglu amesema mwili wake umehifadhiwa kwa misingi ya dini ya Orthodox.
Rubani mwenza Konstantin Murakhtin alinusurika na akapatikana akiwa hai katika operesheni ya maafisa wa kitengo maalum cha Urusi na majeshi ya Syria.
Katika operesheni hiyo Helikopta moja ya kijeshi ya Urusi pia ilidunguliwa huku afisa mmoja wa kitengo maalum cha jeshi ya urusi akipoteza maisha yake.
Licha ya hayo kapteni Konstantin Murakhtin ameomba ruhusa arejee Syria iliakalipize kisasi cha mauaji ya rubani wake Oleg Peshkov.



Image copyright
Rais Putina anataka Uturuki iombe msamaha kwa kuangusha ndege yake

Tukio hilo la kuangushwa kwa ndege hiyo juma lililopita limesababisha uhasama kuibuka baina ya mataifa hayo ambayo kitambo yalikuwa washirika wa karibi.
Mataifa hayo mawili yanayounga mkono makundi hasimu yanayopigana nchini Syria.
Urusi inamuunga mkono rais Bashar al Assad na majeshi yake huku Uturuki ikiwaunga mkono waasi wanaotaka kumpindua rais Assad.
Mnamo siku ya jumamosi Urusi ilitangaza vikwazo kadhaa vya kiuchumi dhidi ya Uturuki ikisisitiza kuwa Uturuki sharti iombe msamaha kwa kuangusha ndege hiyo ilhali ilikuwa katika anga ya Syria.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekataa kuomba msamaha kufuatia shambulizi hilo lililoiudhi Urusi.
Source: www.bbc.com/swahili/
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment