DC MAKONDA AKERWA NA MALIPO TATA YA SHS. 5.7 BILIONI



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda 
By Tumaini Msowoya
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amekerwa na malipo tata ya Sh5.7 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara tano zilizojengwa kwenye wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Makonda malipo halisi ya ujenzi wa barabara kwa mujibu wa mkataba yalikuwa Sh4.9 bilioni, lakini wakati walipaji waliongeza ‘chajuu’kiasi cha Sh800 milioni.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo, Makonda alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa hiyo, Ando Mwankuga kuwachukulia hatua stahiki za kisheria wote waliohusika katika kuidhinisha malipo hayo, wakiwemo wakandarasi.
Agizo la Makonda linakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Muhagama kumtaka Mwankuga ampe taarifa ya ujenzi wa mfereji wa Tegeta-Basihaya, uliojengwa chini ya kiwango na kusababisha mafuriko.
Mhagama alimtaka Mwankuga kuwachukulia hatua za kisheria wahandisi aliowaita ‘mizigo’ kwa madai ya kushindwa kusimamia miradi muhimu ya maendeleo kwenye manispaa hiyo.
“Kinachosikitisha zaidi ni kwamba barabara moja iliyotakiwa kulipwa Sh592 milioni imeongezewa hadi kufikia Sh800 milioni kinyume kabisa cha utaratibu. Bodi ya wazabuni ilipoenda kukagua miradi hii ikakuta tayari malipo yameshafanyika wakati ambapo mfuko wa barabara ulizuia yasifanyike,” alisema Makonda.
Alizitaja barabara hizo kuwa ni Mkwajuni-Mago iliyotakiwa kulipwa Sh404.1 milioni lakini imeongezeka na kufikia Sh617.6 milioni, Maandazi Sh799.01 hadi Sh1.2 bilioni na Lion Sh592.07 lakini imelipwa Sh860.1.
Barabara nyingine ni Mabatini iliyotakiwa kulipwa Sh655.5 milioni lakini imeongezeka hadi kufikia 777.8 milioni na Journalism-Feza Sh1.8 Bilioni hadi 2.006.
Makonda aliwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.
Mwananchi
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment