MAKALA YA SHERIA: JE KULEWA, KUTOKUWA NA AKILI TIMAMU NI KINGA BAADA YA KUTENDA JINAI
DEC182015
Na Bashir Yakub.
Wote tunajua kuwa kila atendaye kosa sharti aadhibiwe. Na kuadhibiwa huko lazima kuwe kwa mujibu wa sheria. Pamoja na kuwa mtenda kosa hustahili adhabu bado watenda kosa hutofautiana hadhi. Hadhi hapa sio kuwa fulani ni mkuu wa mkoa au mkurugenzi na fulani ni mkulima wa kawaida kijijini Katanakya.
Hadhi ndio kama hizo zilizotajwa katika kichwa cha makala. Wapo watenda makosa lakini wakiwa na umri mdogo, wapo watenda makosa lakini wakiwa hawana akili timamu halikadhalika wapo watenda makosa lakini wakiwa na akili isiyo ya kawaida kwa maana ya akili ya ulevi.
Sheria inasemaje kuhusu hawa wote kuanzia utendaji wao makosa, kushitakiwa na kuwajibika kwao. Makala yataeleza ili tujue hadhi ya kimashitaka ya makundi haya.
1.JE MWENYE UGONJWA WA AKILI ANAWEZA KUSHITAKIWA ?.
Jibu ni ndiyo sheria haikatazi kumshitaki mwenye ugonjwa wa akili( chizi). Kuna tofauti kati ya kushitakiwa na kuwajibika. Kushitakiwa ni kumfungulia mashtaka na kuwajibika ni kupata adhabu baada ya kupatikana na hatia. Kwa hiyo kushitakiwa atashitakiwa isipokuwa sheria inatoa mwongozo kuhusu kuwajibika kwake.
Kifungu cha 13 ( 1 ) cha Kanuni za adhabu sura ya 16 kinasema kuwa mtu hatawajibika kwa kutenda kosa la jinai iwapo wakati wa kutenda kitendo hicho alikuwa katika hali ya ugonjwa wowote unaoathiri akili yake. Hiyo ni kanuni ya jumla iliyowekwa na kifungu hicho.
Hata hivyo kifungu hichohicho kimeweka masharti kuwa yapo mazingira ambayo mwenye ugonjwa wa akili atatakiwa kuwajibika. Kinasema kuwa mwenye ugonjwa wa akili hatawajibika kwa kutenda kosa la jinai iwapo tu wakati anatenda kosa alikuwa hajui anachokitenda, hana uwezo wa kutambua kuwa hapaswi kutenda kosa, na hana uwezo wa kuzuia kitendo hicho.
Hii maana yake ni kuwa ikiwa mgonjwa wa akili anao uwezo wa kujitambua wakati akitenda kosa basi atapatikana na jinai hata kama ameua kwa makusudi atahukumiwa kunyongwa. Maswali ya kitaalam(examination) atakayoulizwa mahakamani ndiyo yatakayotoa majibu ikiwa alikuwa anajitambua wakati wa kutenda kosa au lah. Hii ni kwasababu akademia ya tiba inaonesha kuwa machizi wengi si wakati wote huwa hawajitambui.
ROO YA TATU YA PROMOSHENI YA "JAZA MAFUTA NA USHINDE" YA GAPCO YAFANYIKA JIJINI DAR
DEC182015
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Jane Mwita (kati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwa Wateja wake wa jijini Dar es Salaam,ambapo zaidi ya wateja 25 huibuka kidedea kila wiki. Kulia anaeshuhudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Chiku Saleh na Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.
COPYRIGHT: MTAA KWA MTAA BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO
RAIA WANNE WA CHINA WAHUKUMIWA KUTUMIKIA MIAKA 20 JELA KILA MMOJA KWA UHUJUMU UCHUMI MKOANI MBEYA
DEC182015
Raia wanne wa China ambao wamehukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi mkoani Mbeya.
Washatkiwa wanne wa China wakipanda karandinga baada ya kuhukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Msangi akiwa na maafisa wake pamoj na Pembe za Faru walizokamatwa nazo rai wanne wa China katika mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Na Deo Kakuru wa Globu ya Jamii, Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Msangi akiwa na maafisa wake pamoj na Pembe za Faru walizokamatwa nazo rai wanne wa China katika mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Na Deo Kakuru wa Globu ya Jamii, Mbeya
Raia wanne wa China wamehukumiwa kutumikia jela miaka 20 kila mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Zaidi ya shilingi bilioni 10 baada ya kukutwa na makosa matatu ya kuhujumu uchumi wakati walipokuwa wakisafirisha pembe 11 za Faru katika mpaka wa Kasumulo mkoani Mbeya. Washtakiwa hao ni SONG LEO (33), XIAO SHAODAN (29), CHEN JIANLIN (34) NA HU LIAN (30) ambao walikamatwa Novemba sita huko Kasumulo mpakani mwa Malawi na Tanzania wakijaribu kuingiza pembe hizo kutokea Malawi bila kibali.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na makossa matatu ambayo ni kuongoza na kushiriki makosa ya uhujumu uchumi kinyume na sheria ya wanyamapori ya mwaka 2002.
Kosa la pili ni kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria ya uhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 na kosa la tatu ni kumiliki nyara za serikali kinyume cha seheria hiyo Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Mbeya Michael Mteite ambaye ameeleza kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri hivyo na kuona washtakiwa wanayo kesi ya kujibu.
Hata hivyo Hakimu Mteite ametupilia mbali ombi la upande wa utetezi uliotaka washtakiwa kupunguziwa adhabu na kwamba hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Hii ni kesi ya kwanza kwa hakimu Mteite ambayo amejivunia kuiendesha ndani ya kipindi kifupi cha siku 23 tangu washtakiwa hao walipofikishwa mahakamani hapo Novemba 24 mwaka huu.
Kesi hiyo ambayo imesikilizw kwa Zaidi ya masaa matano imevuta hisia za wakazi wa mkoa wa Mbeya ambao walikuwa wakiifuatilia kwa karibu na kutaka kujua nini hatima yake.
Washtakiwa hao kwa pamoja wamepandishwa kwenye karandinga la polisi tayari kuanza kutumikia adhabu yao gerezani licha ya Hakimu Mteite kueleza kuwa milango ya kukata rufaa iko wazi endapo wataona hawakuridhishwa na hukumu hiyo.
HUDUMA YA KUGAWA DAWA ZA MATENDE NA MABUSHA KUANZA DISEMBA 19 DAR
DEC182015
Na Shamimu Nyaki - Maelezo
Serikali kupitia Mpango wa wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo.
Tamko hilo limetolewa na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto Bw. Donald Mmbando alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.
Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.
“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.
Aidha zoezi hilo litatekelezwa katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga na kutibu magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki itafanya zoezi hilo katika ngazi ya jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari 2016.
Naye Mratibu wa Mpango huo Dkt Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18 imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.
Vile vile Dkt Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.
Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.
JAJI MARK BOMANI AMSHAURI MAALIM SEIF AKUBALI UCHAGUZI URUDIWE
DEC172015
Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.
Boman ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.
“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.
Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.
Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika katika mchakato huo.
Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.
Mtaa kwa Mtaa blog
About Mind 2024
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment