KASI YA RAIS MAGUFULI YATIKISA DUNIA, AWA GUMZO AUSTRALIA

Rais Dkt.John Pombe Magufuli
Rais Dkt.John Pombe Magufuli

Iliandikwa Tarehe December 1, 2015

Kasi ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli ime endelea kuweka rekodi katika maeneo mbalimbali nje ya nchi tangu aapishwe  kuwa rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mara baada ya kuingia madarakani  Rais Magufuli amefuta safari za nje kwa watumishi wa umma ili fedha hizo zikasaidie katika shughuli nyingine za maendeleo kwa wananchi, amefuta sherehe za uhuru, siku ya Ukimwi Duniani, uchapishaji wa kadi sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya, kuagiza fedha za sherehe za Wabunge kununulia Vitanda pamoja kuwasimamisha kazi vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutokana na sakata la upotevu makontena 349 yaliyopelekea hasara  ya zaidi ya Bilioni 80.
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyopandisha rekodi ya utendaji wa  Rais Magufuli Duniani kutokana na maamuzi magumu yaliyoweza kuokoa fedha nyingi ambazo zitasaidi katika kupeleka huduma moja kwa moja kwa wananchi.
Baadhi ya nchi ambazo Rais Magufuli amekuwa gumzo ni pamoja na nchi ya Marekani ambapo Gazeti kubwa la Marekani, The Guardian limeandika habari isemayo: What would Tanzania’s cost-cutting president do?.
Licha ya hilo gazeti kubwa,nchini Australia pia Rais Magufuli amekuwa gumzo kufuatia gazeti kubwa la  The Courier-Mail kuandika makala ndefu likimtaka Waziri mkuu wao,  Malcolm Turnbull ajifunze achapakazi toka kwa Rais wa Tanzania,Dr John Pombe Magufuli.
Kwa upande mwingine  katika mitando ya kijamii katika nchi za Nigeria, Kenya Afrika Kusini na sehemu nyingine Rais Magufuli amekuwa gumzo huku baadhi ya raia katika  nchi hizo wakitamani kuwa na kiongozi wa aina ya Magufuli.
Haya ni baadhi ya magazeti ya nje ya nchi yaliyo ripoti habari za utendaji kazi na kasi ya Rais Magufuli.
kio
Source: hivisasa.co.tz
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment