KIMENUKA TENA BANDARINI, MAKONTENA 2431 "YAOTA MBAWA", WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA TENA YA KUSHTUKIZA ATAKA MAJIBU KABLA YA JUA KUZAMA


Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na K-Vis Media
ULE “moto” aliouwasha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Kassim Majaliwa kwenye bandari ya Dar es Salaam wiki iliyopita, na kukolezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kumsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw.  Rished Bade, umeendelea kusambaa kwenye eneo lote la bandari na viunga vyake baada ya leo tena Bw. Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta makontena mengine 2431yenye bidhaa  hayajulikani yaliko.

Baada ya kugundua hilo tena kwa ushahidi wa nyaraka, Waziri Mkuu ambaye wiki iliyopita aliahidi kuwa "Tunataka ku-deal na wajanja wajanja wa TRA." ameagiza uongozi wa bandari ya Dar es Salaam, kuwasilisha ripoti kamili ya waliokula dili kabla ya jua kuzama leo hii Desemba 3, 2015, "Saa 11 jioni ya leo nahitaji ripoti kamili ofisini kwangu" Aliagiza Waziri Mkuu. Wakati wiki iliyopita Waziri Mkuu alikula sahani moja na watu wa TRA, leo hii kibao kimewageukia Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, bandari ya Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kusafisha na kuondoa “uhuni” huo uliokuwa ukifanywa kwa muda mrefu na kygeuka kuwa tabia ya watumishi wa umma. Moto huo haukuishia hapo,  Waziri Mkuu pia alifanya ziara kama hiyo pale stesheni kuu ya reli iliyo chini ya Kampuni ya Reli Tanzania TRL na kukuta mambo ni "ulaji" tu ambapo TRL ilipatiwa fedha takriban bilioni 3 ili kujitutumua na kujiendesha yenyewe, badala yake fedha hizo hazikufanya chochote cha maana na kuishia kulipana posho na mishahara kwa "vigogo".



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo  Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali.(Picha na Ofisi ya Waziri )


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu,  Kassim Majliwa  akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea stesheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hii ndiyo bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa takriban wiki mbili sasa, imekuwa gumzo kwa wakazi wa jiji na nchi jirani baada ya Utawala wa serikali ya awamu ya tano kuanzisha "fagio" la chuma. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

Source: Khalfansaid.blogspot.com
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment