NEW YORK, MAREKANI
MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani kutoka kundi la Young Money Records, Nick Minaj, amefanikiwa kumtoa kaka yake, Jelani Miraj, kifungoni baada ya kulipa dola 100,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 200.
Jelani alipelekwa jela kutokana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12, ambapo alianza kukitumikia kifungo tangu Aprili mwaka huu, lakini msanii huyo alifanikiwa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kaka yake.
Nick amekuwa akifanya makubwa kwa kaka yake ambapo kabla ya kwenda jela, Nick alitoa mchango wa harusi ya kaka yake huyo wenye thamani ya dola 30,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 60.
Hata hivyo, msanii huyo alizidi kuonyesha upendo wa dhati kwa kaka yake ambapo alimpa nyumba kwa ajili ya kuishi na mke wake mara baada ya kufunga ndoa.
Source: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment