POLISI YAWAANGUKIA ABIRIA KUDHIBITI AJALI

POLISI mkoani Katavi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani imezindua kampeni inayowataka abiria kushirikiana kudhibiti na kupunguza ajali za barabarani hasa kipindi cha kuelekea siku za Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Uzinduzi wa kampeni hiyo ya ‘abiria paza sauti’, ulifanyika jana. Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani, mkoa wa Katavi , Joseph Mfinanga pamoja na maofisa wa Usalama Barabarani, walitoa elimu kwa abiria wa mabasi ya masafa marefu juu ya wajibu na haki zao wanapokuwa safarini.
Walipanda mabasi tofauti yaendayo nje ya mkoa huo kuanzia Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Mpanda na kuelimisha abiria umuhimu wa abiria kufunga mikanda wanapokuwa safarini. Pia waliwaelimisha kuhakikisha wanakuwa na tiketi yenye majina yao, kampuni ya basi, namba ya kiti na haki ya kudai nauli pale gari linapoharibika.
Katibu wa waendesha vyombo vya moto Mkoa wa Katavi, Nassoro Arfi aliwaasa abiria kutumia simu zao za mkononi kutoa taarifa iwapo wahudumu wa mabasi ya abiria watakuwa wakitumia lugha chafu.
Alitoa namba ya simu 068288772 kwa abiria iwapo watakutwa na tatizo safarini . Hata hivyo, baadhi ya madereva na makondakta walisema tatizo la mwendo kasi wakati mwingine linasababishwa na abiria ambao huwataka waendeshe magari kwa mwendo kasi.
Habaari Leo



Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment