Dr. Wilbroad Slaa
KASI ya kupambana na ufisadi ya Rais Dk. John Magufuli, imefufua matumaini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, kuhusu hatma ya Tanzania.
Hata hivyo Dk. Slaa amesema bila kuifumua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) matarajio ya Watanzania yanaweza yasifikiwe.
Slaa ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kama kiongozi anayepambana na rushwa kwa nguvu zote, ameliambia Raia Mwema mwanzoni mwa wiki hii kwamba, Tanzania kwa sasa inahitaji Rais aina ya Magufuli na kuwataka wananchi wamuunge mkono katika juhudi za kusafisha nchi.
“Nadhani unaelewa sasa niliposhikilia msimamo wangu, katika mazingira ya sasa Magufuli is the best (ni bora zaidi). Kumbuka nyuma niliwahi kusema nchi hii kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kurudisha kwenye mstari ulionyooka! Nimefurashi sana,” alisema Dk Slaa.
Akizungumzia baadhi ya madai ya watu kwamba kasi hii inaweza kujenga misingi ya uongozi wa kidikteta na kwamba inaweza kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi, alisema kwa jinsi ufisadi ulivyokita mizizi kwenye mfumo wa nchi zinahitajika hatua za namna hiyo kupambana nao. “Aliahidi, anatekeleza sasa wanataka nini! Udhibitiwe (udikteta) na Bunge ili usipindukie mipaka, lakini tusilalamike tu,” alisema.
Dk. Slaa ambaye alikuwa mwiba kwa Serikali ya CCM, hasa katika Awamu ya Tatu, kwa kulipua aliyoyaita mabomu ya vitendo vya ufisadi wa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma, alishauri ili kasi ya rais iweze kupata mwendelezo mzuri kwenye vita dhidi ya rushwa, ni lazima Takukuru isukwe upya. “Pasipo kuchukua hatua ya kufumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa.
Dk. Slaa ambaye alikuwa mwiba kwa Serikali ya CCM, hasa katika Awamu ya Tatu, kwa kulipua aliyoyaita mabomu ya vitendo vya ufisadi wa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma, alishauri ili kasi ya rais iweze kupata mwendelezo mzuri kwenye vita dhidi ya rushwa, ni lazima Takukuru isukwe upya. “Pasipo kuchukua hatua ya kufumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa.
Naona inatakiwa hatua ya haraka kwa Takukuru,” alisema Slaa. Wabunge waingiwa hofu.
Wakati Slaa akipongeza hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli, baadhi ya wabunge wa CCM wanahofia kusema neno lolote kuhusu juhudi hizo.
“Kazi anafanya nzuri na sisi tunaipenda, lakini sasa ukiomba maoni yangu hadharani naweza kuambiwa najipendekeza kutafuta cheo na jamaa, hataki kusikia anapewa sifa za kujipendekeza,” alisema mbunge mmoja maarufu na kuongeza; “Haya masuala ya makontena tuliyasemea sana bungeni lakini tulionekana wasaliti na wapinzani, lakini kipindi hiki ukipongeza pamoja na hatua nzuri zinazochukuliwa na Rais tutaonekana tunajipendekeza ili tuteuliwe kuwa mawaziri.”
Tangu akabidhiwe majukumu ya Ikulu baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Magufuli ni pamoja kutembelea Wizara ya Fedha na kujionea hali halisi kwa baadhi ya watumishi kukosekana ofisini saa za kazi, kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kujionea udhaifu wa kiutendaji uliopo hospitalini hapo na kuvunja Bodi ya Hospitali ya hiyo na kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto.
Mbali na Kidanto, tayari Magufuli amekwishamsimamisha kazi na kuamuru kuchunguzwa kwa aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade, Kamishna wa Forodha Tiagi Masamaki, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Habibu Mponezya.
Wengine waliosimamishwa kazi ni Harun Mpambe wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Kitengo cha Bandari Kavu (ICD), Eliachi Mrema, Nsajigwa Mwandegele , Robert Nyoni na Anangise Mtafya.
Akitangaza uamuzi huo kwa waandishi wa habari, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema Rais pia amezuia safari kwa watumishi wote wa TRA ili watoe ushirikiano katika uchunguzi wa sakata hilo.
“Mnakumbuka kuwa Rais alisema atatumbua majipu, hilo ni jipu la kwanza lakini bado uchunguzi unaendelea. Watasimamishwa zaidi kadri uchunguzi unavyoendelea,” alisema Sefue.
Source: Raia Mwema
0 comments:
Post a Comment