'SERIKALI IZIBE PENGO LA UHABA WA MADAKTARI'

RAIS mstaafu, Alhaji Hassan Mwinyi (pichani), ameshauri serikali kufanya jitihada kubwa kuhakikisha inaziba pengo la uhaba wa madaktari na wauguzi kuokoa afya za Watanzania. Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afya na Teknolojia (IMTU), yaliyofanyika chuoni hapo.
Katika mahafali hayo ya nane, madaktari 148 walihitimu Shahada ya Udaktari, wahitimu 19 Shahada ya Uuguzi na kumi walitunukiwa vyeti na Stashahada za uuguzi. “Kwa mfano wenzetu nchini Marekani daktari mmoja anahudumia wastani wa wagonjwa 400 kwa mwaka wakati hapa kwetu daktari mmoja anahudumia wagonjwa 40,000…hili ni pengo kubwa sana ambalo tunapaswa kuliziba haraka,” alisema.
Alisifu chuo hicho kuzalisha wahitimu wa udaktari na uuguzi. “Ili tuweze kupunguza pengo la wataalamu hawa, taasisi binafsi kama IMTU ni muhimu sana maana watatusaidia kutengeneza wataalamu vijana ambao watakwenda kuwahudumia wenzao huko vijijini na mijini,” alisema.
Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Yunus Mgaya, alipongeza chuo hicho na wote waliosababisha kiweze kutoa wahitimu bora na kuendelea kuwa imara kitaaluma.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Brhamanaidu Katuri, alisema uhusiano wa Tanzania na India ni wa muda mrefu hasa katika nyanja za elimu, afya, uchumi na katika maeneo ya utamaduni.
“Uhusiano huu baina ya India na Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kwa pande hizi na tutaendelea kuhakikisha unadumu kwa manufaa ya wananchi wa pande hizi mbili….nakuhakikishia IMTU itaendelea kutoa wahitimu bora wa udaktari na uuguzi,”
Source: Habari Leo
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment