BADILISHA MAWAZO YAKO HARAKA HUU NI MWAKA 2016 USIISHI KWA MAZOEA...........
Lazima miongoni mwetu tutakua kati ya hawa.
Hujawahi fikiria kama biashara ya maandazi ina hela sana hadi ulivyoona Baresa anauza,
Unakunywa bia kila mwezi lakini huna plan ya kufanya savings,
Umeshahudhuria mara nyingi sana vikao vya harusi na kuchangia lakini hujawahi hudhuria seminar za ujasiliamali,
Unatumia smart phone lakini kila siku unalalamika huna hela ya mtaji,
Unajua kumbi gani za starehe zinajaza sana lakini hujui ni biashara ipi unaweza ifanya kulingana na uwezo wako,
Kila Ukiwa social networks unajihusisha Sana na mambo yasiyo na manufaa ya kifedha kuliko yenye manufaa ya kifedha . ,
Kwako ni rahisi sana kusambaza msg kama vile za Anna Kansiime na Mkude Simba kuliko kama hii,
Tangu unapata mshahara wa laki tatu hadi sasa wa milioni mbili bado mshahara haukutoshi,
Unajua Beyonce katoa album gani, ana date na nani, anavaa nguo za nembo gani lakini hujui watu wanapataje hela kwenye masoko ya hisa,
Kila siku unaweza ukipata hela "isiyo na kazi" utanunua smartphone toleo jipya badala ya
Ya kuifanyia shughuli za kukuongezea kipato,
Ya kuifanyia shughuli za kukuongezea kipato,
Kwako ni rahisi kukopa hela ya kumpa rafiki yake na shemeji yako kuliko kukopa hela na kufanya biashara ndogo.. ,
Biashara akiifanya mtu mwingine ni rahisi kuliko ukifanya wewe,
kwako ni rahisi kumuamini mtu anaekwambia 'ukitaka kuwa tajiri mtegemee Mungu' kuliko yule anaekwambia 'its not in God's plan to make you rich!',
Ukiwa unaangalia taarifa ya habari, unaishia za kitaifa tu au na za kimataifa, habari za kibiashara hazina
umuhimu kwako,
umuhimu kwako,
Uko radhi kutoka Mbagala Chalambe hadi Tegeta kumsalimia mpenzi wako lakini Chalambe hadi ubungo kwenye seminar ya ujasilamali ni mbali sana kwako,
Unajua Diamond anaendesha gari la bei gani, Gwajima analipwa kiasi gani, msanii gani kafilisika, movie ya Ray ya mwisho iliingiza kiasi gani lakini hujui matumizi yako kwa mwezi ni kiasi gani,
Mtu akikuletea kadi ya mchango wa harusi ni rahisi kuchangia kuliko anae leta mchango wa ada,
Kwenye whasapp groups unachangia sana maswala ya skendo, utani, fumanizi, mahaba, kejeli na kutumia muda mwingi sana kusoma au kuangalia mambo hayo kuliko mambo ya kutafuta hela, (Infact msg kama hizi zinakukera sana sababu kwanza hazikuchekeshi halafu ni ndefu!)
vitu kama fursa za kibiashara, ujasiliamali, mchanganuo wa kibiashara hua unavisikia tu, hujawahi kuvitafuta au kufanyia kazi,. .
Kile kikao chenu cha kuanzisha kikundi cha huweka na kukopeshana hela mlichopanga tangu mwaka jana hakijatokea lakini vikao vyote vya kukutana bar vimetokea, vingine bila hata kupangwa!!..
Mtu akikualika kwenye kufanya biashara unaona anataka kukutapeli, lakini anaekualika kwenye kula bata ndo wa ukweli....
2016 Tafakari chukua hatua Uwe tofauti!
0 comments:
Post a Comment