HABARI MBALIMBALI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

DKT SHEIN ATOA SALAMU KWA WANANCHI KUKARIBISHA MWAKA MPYA NA HABARI ZINGINE KUPITIA SIMU TV



Wachezaji wa klabu ya Simba jana wamelionja joto la jiwe baada ya mashabiki wa Ndanda FC kuwavamia wachezaji wakati wa mazoezi.  https://youtu.be/6kqjr9XjQ00

Timu ya CDA imetupwa nje katika mashindano ya kombe la shirikisho baada ya kupokea kichapo cha bao 1 toka kwa Singida United.  https://youtu.be/KmxQHdfWOqU
Serikali imetoa tamko kuwa itaendelea kuwalipa mishahara makocha wote  wa timu za taifa   https://youtu.be/Ochi73k6Q64
Fahamu mengi kutoka kwa Mch. Samwel Maela akikufundisha mengi kuhusu mpango wa Mungu na taifa la Tanzania mwaka 2016: https://youtu.be/rO96gpssLDs

Jionee mengi jinsi watanzania wanavyosherekea kwa furaha mwaka mpya na wakizungumza  matarajio yao kwa mwaka mpya mwaka 2016:https://youtu.be/A7jcptFyuAw

Kutana na wachambuzi wa masuala ya maendeleo kutoka visiwani Zanzibar wakikuelimisha mambo kadha wa kadha kuhusu ujenzi wa taifa:https://youtu.be/1SVUJ6ElmDA

Msikilize Mkurugenzi wa gesi kwa matumizi ya nyumbani akikuhabarisha kuhusu usambazaji na matumizi ya gesi majumbani:  https://youtu.be/MtYkLmdwXW8

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi mhe. Lukuvi awaongoza wakazi wa jiji la Dar katika mkesha wa mwaka mpya.   https://youtu.be/HIk94oLcmNc

Serikali yaahidi kuwawekea walemavu mpango maalumu ili kuwatengezea mazingira bora ya ajira.   https://youtu.be/GH9uvGzSIAk

Jeshi la polisi mkoani Simiyu limekamata gari aina ya Toyota Harrier lililoibiwa December 7 jijini Dar   https://youtu.be/Z17Ly6KRuBY

Kamishna Suleiman Kova aliyekuwa mkuu wa kanda maalumu ya Dar es Salaam amestaafu kulitumikia jeshi la polisi.   https://youtu.be/u5xOJa44sRQ



  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
 Waziri akiwa katika picha ya pamoja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
Waziri waWizara ya Ujenzi,. Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prtof Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni katika jingo la kikosi cha zimamoto cha kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA WA MKESHA WA MWAKA 2016 KATIKA PICHA

 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyakea wakiwa katika mkesha wa mwaka mpya.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na mkewe wakicheza kwa furaha wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiwa na furaha wakati wa mkesha wa mwaka 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye(katikati) akicheza nyimbo za injili wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha wa Kuliombea Taifa (Dua maalum), Mchungaji Godfrey Mallassu akizungumza katika mkesha huo.

HAWA NDIO MAJENERALI WALIOTEULIWA KUWA MAKATIBU WAKUU WIZARA ZA MALIASILI NA UTALII NA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wakisubiri zamu zao za kula kiapo mbele ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi (kushoto) na Jaji, Wakili Mkuu Meja Jenerali Projest Anatory Rwegasira Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016. Picha na IKULU
WAZIRI MKUU  Mhe. Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, mara baada ya kuapishwa Ikulu  jijini Dar es Salaam leo. 
Ametoa pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
Mhe. Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na  kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na  Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa wakati wa Kampeni.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
 Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, baada ya  viongozi hao kutia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu  jijini Dar es Salaam leo January 1, 2016

  Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, baada ya  viongozi hao kutia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu  jijini Dar es Salaam leo January 1, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju wakishuhudia Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju wakishuhudia Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakiapa kabla ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016. PICHA NA IKULU

MICHUZI BLOG

Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment