Kwa namna ya pekee sana ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mungu kwa neema na rehema zake zilizo kuu kwangu. Pamoja na misukosuko mingi ya maisha, leo ikiwa ni siku yangu ya kuzaliwa, napenda niseme tu kwamba 'Acheni Mungu aitwe Mungu'.
Hivyo, nichukue fursa hii adhimu kumshukuru Mungu kuniwezesha kuiona siku ya leo January, 01.
Happy Birthday to Me
Pamoja na salamu hizi za siku ya kuzaliwa kwangu, napenda niwatakie heri watu wote, ikiwa ni pamoja na wagonjwa walio mahospitalini na majumbani, wafanyakazi, wanafunzi, walemavu wa aina zote, viongozi wa serikali, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, sekta binafsi na wengine ambao pengine nimewasahau.
Heri ya Mwaka Mpya wa 2016
Kipekee namtakia heri ya mwaka mpya
Rais wetu Mh. Dkt. John Pombe Magufuli
na
cabinet yake,
Mungu awape afya njema na uongozi imara utakaoleta matumaini mapya kwa watanzania.
Mungu ibariki Tanzania
0 comments:
Post a Comment