JPM AWAKUNA WANANCHI WENYE ULEMAVU, WAMSHUKURU KWA KUTIMIZA AHADI YA KUWAKUMBUKA KATIKA UONGOZI WAKE

JPM AWAKUNA WANANCHI WENYE ULEMAVU, WAMSHUKURU KWA KUTIMIZA AHADI YA KUWAKUMBUKA KATIKA UONGOZI WAKE

Na Sultani Kipingo Alianza na Dkt. Abdallah Possi, wakafuata Profesa James Epiphan Mdoe na Mhe. Amon Anastaz Mpanju na kusababisha mshangao wa furaha miongoni mwa wananchi wenye ulemavu kwa kile wanachokitaja kama kukumbukwa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 
Rais alipomteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu wengi walifurahi kuona Mtanzania wa kwanza mwenye ualbino anaingia katika Baraza la Mawaziri 
Furaha hiyo ilizidi alipowatea Mhe. Amon Anastaz Mpanju mlemavu wa kuona kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria na Profesa James James Epiphan Mdoe kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, ambaye ni mlemavu wa miguu.
 Mhe Mpanju, ambaye kitaaluma ni mwanasheria na ambaye pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa Bunge la Katiba, alishangaza kila mtu wakati alipokula kiapo mbele ya Rais bila kusoma mahali kama ilivyo desturi. 
“Huyu bwana pamoja na ulemavu wake hakika ni mtu wa kazi” alisikika mmoja wa wageni waliohudhuria hafla ya kuapishwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu siku ya Mwaka mpya. 
Akiwa amesindikizwa na mke wake, Mhe. Mpanju alipokea Biblia Takatifu na kuinyanyua juu na kuanza kula kiapo, ingawa mkewe alikuwa ameshika karatasi ya maandiko ya vitoneambayo ilikuwa aitumie. Hata Rais alitabasamu kwa hilo. 
Huko mitaani, ambako tukio hilo la kuapishwa Makatibu wakuu lilikuwa likirushwa ‘live’ na vituo kadhaa vya TV na Redio na mitandao, wengi walishikwa na butwaa, huku wakimsifia Rais Magufuli kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu. 
Waliendelea kufurahi walipomuona Profesa James James Epiphan Mdoe, ambaye ni msomi aliyebobea katika Kemia,  akisogea mbele kwa mikongojo miwili na kula kiapo cha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini. 
“Tingatinga (Rais Magufuli) ametukuna kweli kwa uteuzi wa viongozi hawa”, mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Gaddy aliiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu kutokea mjini Iringa. Gaddy, ambaye yeye ni mlemavu wa miguu, amesema kitendo cha kuteua wananchi wenye ulemavu kushika madarka ya juu serikalini kimewapa furaha na faraja kubwa kiasi hata yeye anajisikia ana cheo tayari. 
Mwananchi mwingine wa mjini Lindi aliyesema anaitwa Mohamed Mpanyachi alipiga simu na kusema kwamba anategemea Rais Magufuli ataendelea kuwapa nafasi walemavu katika ngazi mbalimbali kwani kama walivyo hao watatu, wananchi wenye ulemavu ambao ni wasomi na wenye uwezo wa kuongoza wamejaa kila pembe nchini.
 Dkt. Abdallah Possi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu - siku alipoapishwa rasmi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 13, 2015
 Profesa James James Epiphan Mdoe akila kiapo kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mbele ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Amon Anastaz Mpanju akiongozwa na msaidizi wake kujiunga na viongozi wenzie ili kutia saini Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma  mbele ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment