KAMATI ZA BUNGE HADHARANI LEO

jobNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kutangaza kamati za Bunge leo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ndugai alisema atatangaza kamati hizo chini ya utaratibu mpya na kwamba leo atatangaza Kamati ya Kanuni pekee.
Baada ya kuitangaza kamati hiyo, nyingine zilizobaki atazitangazia mjini Dodoma wakati vikao vya Bunge vitakapokuwa vikiendelea mwishoni mwa mwezi huu.
Utaratibu huo umebainishwa na Ndugai alipoulizwa na gazeti hili ambalo lilitaka kujua iwapo Kamati za Bunge zitatangazwa kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo Januari 26, Mwaka huu.
“Kesho (Leo) nitatangaza kamati moja tu ya kanuni na nyingine nitazitangazia mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo,” alijibu kwa ufupi.
Taarifa ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema kwamba Spika Ndugai amepanga kupunguza wingi wa Kamati za Bunge ili kuendana na uchache wa wizara zilizopo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kamati zinakuwa chache lakini zilizo na uwezo wa kufanyakazi kwa kasi ambayo itaisaidia serikali ya awamu ya tano.
Baada ya leo kutangaza Kamati ya Kanuni, Spika Ndugai atabaki na jukumu la kutangaza kamati nyingine 14 mjini Dodoma, iwapo hakutakuwa na ongezeko la kamati.
Kamati za Bunge huundwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 96, likiwa limepewa madaraka ya kuunda kamati za Bunge za aina mbalimbali na muundo wake umefafanuliwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.
Katika muundo huo zipo kamati za kisekta na zile zisizokuwa za kisekta, ambazo kwa pamoja hufanyakazi na kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya Bunge.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 89 Bunge limeunda Kamati 15, ambapo baadhi ya kamati hizo ni Kamati ya Haki, Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
Mtanzania
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment