NA SOMOE NG`ITU
11th January 2016
Ni baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar, ambayo sasa itacheza fainali ya michuano hiyo kwa mara tano tangu ilipoanzishwa...
Kwa matokeo hayo, Mtibwa imetinga fainali ya michuano hiyo, ikiwa ni mara ya tano baada ya kufanya hivyo mwaka, 2007, 2008, 2010 (walitwaa ubingwa), 2015 na mwaka huu.
Miaka miwili iliyopita, mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Simba walifanikiwa kufika hatua ya fainali, wakipoteza dhidi ya KCC ya Uganda mwaka 2014 kabla ya kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 katika fainali ya mwaka jana.
Jeba alifunga bao hilo muhimu katika dakika ya 45 akimalizia kwenye kamba mpira uliotemwa na kipa wa Simba, Manyika Peter kufuatia shuti la mguu wa kushoto ndani ya boksi lililopigwa na kinda Shiza Kichuya (19).
Bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Jeba baada ya kucheza mechi tatu za Kundi B la michuano hiyo bila kutikisa kamba.
Katika mchezo huo, mabingwa Simba walipoteza nafasi kadhaa za kufunga kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Mtibwa.
Dakika ya 11 Mussa Hassan ' Mgosi' akiwa ndani ya 18 alichelewa kuunganisha krosi ya Mwinyi Kazimoto na kumpa nafasi beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daudi kuokoa hatari hiyo langoni mwao.
Mtibwa wangeweza kuongeza bao jingine katika dakika ya 55 kama siyo shuti la Kichuya kukosa shahaba langoni mwa Simba.
Danny Lyanga alikaribia kufunga kwa upande wa Simba katika dakika ya 72 baada ya shuti lake kuokolewa na kipa Said Mohammed kufuatia krosi ya Justice Majabvi.
Ibrahim Rajab 'Jeba' anaifungia Mtibwa Sugar bao la kwanza baada ya kuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Simba, Peter Manyika aliyeshindwa kudaka shuti la Hussein Javu katika dakika ya 45.
Mtibwa Sugar walijibu shambulio hilo katika dakika ya 22 kupitia Jeba aliyeshindwa kufunga akiwa peke yake na kipa wa Simba.
Vikosi vilikuwa:
Simba : Peter Manyika, Emery Nimuboma / Said Ndemla (dk 46), Mohammed Hussein 'Tshabalala', Hassan Isiihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Awadhi Juma/ Ibrahib Ajib, Jonas Mkude, Mussa Hassan Mgosi / Brian Majwega (dk 46), Danny Lyanga na Mwinyi Kazimoto.
Mtibwa Sugar: Said Mohammed, Shabani Nditi, Ally Shomary, Issa Rajab ' Baba Ubaya', Dickson Daudi, Salim Mbonde, Mohammed Ibrahim, Muzammir Yassin, Hussein Javu , Ibrahim Rajab ' Jeba' na Shiza Kichuya.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment