POLISI ADAIWA KUMUUA RAFIKI YAKE KWA KIPIGO

Kamada wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus

Kamada wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha. 
By Jesse Mikofu, Mwananchi
Mwanza. Askari wa kikosi cha Mbwa na Farasi wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, anadaiwa kumuua rafiki yake akiwa amemfunga pingu miguuni baada ya kumtuhumu kumuibia kadi za benki na pochi.
Akizungumza ofisini kwake jana, Kamada wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita na alimtaja alimtaja aliyeuawa kuwa ni Donald Magalata (30) aliyekuwa akifanya kazi ya ulinzi Mwanza Hoteli.
Alisema mauaji hayo yalifanyika nyumbani kwa mtuhimwa alitelekeza ndani ya Kambi ya Polisi eneo la Mabatini.
Alisema siku ya tukio, inadaiwa mtuhumiwa aliporudi kutoka kazini, alikuta baadhi ya vitu vyake havipo kwenye suruali aliyokuwa amevihifadhi, ndipo alimfungia chumbani marehemu nyumbani kwake na kuanza kumshambulia kwa kipigo.
Alisema alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.
“Askari huyo baada ya kutoka kazini siku hiyo saa moja asubuhi, alifika nyumbani kwake na kumkuta amelala ndani, ni rafiki yake aliyekuwa akimsaidia mambo mengi ikiwamo kazi za nyumbani,” alisema kamanda huyo.
“Alipoingia ndani, alibaini kuwa, pochi yake iliyokuwa na vitu vyake ambavyo ni pamoja na kadi mbili za benki na kitambulisho cha kazi havipo, alipomuuliza, hakumpa jibu la kueleweka ndipo mzozo ulianza na mtuhumiwa akaamua kumfunga pingu miguuni huku akimpiga kwa fimbo.”
Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na polisi na uchunguzi bado unaendelea kabla ya kumfikisha mahakamani.
Katika tukio lingine; mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ngereja Mashenene (30) mkazi wa Izunge Bwiro wilayani Ukerewe, ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Mwananchi
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment