Anaedaiwa kumuua Mama yake Marekani akamatwa DSM
By Pascal Mwakyoma TZA, December 24, 2021
Wyluva Ngongoseke, Mwanadada wa Kitanzania ambaye mama yake mzazi Catherine Ngongoseke (60) amekutwa akiwa ameuwawa kwa kuchomwa visu nyumbani kwake Texas nchini Marekani, ndiye mtuhumiwa wa kwanza katika mauaji hayo.
Mwanadada huyo anahisiwa kufanya mauaji hayo na kukimbilia Dar es Salaam, Tanzania kujificha.
Mpaka sasa vyombo vya usalama vya nchini Marekani kwa kushirikiana na polisi wa Tanzania wamefanikiwa kumkamata mwanadada huyo Jijini Dar es Salaam na wapo kwenye mpango wa kumrudisha nchini Marekani kuzikabili tuhuma hizo.
0 comments:
Post a Comment