NA SOMOE NG`ITU
11th January 2016
Akizungumza jana, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa alisema kuwa amempa nafasi hiyo Samatta kutokana na mafanikio makubwa aliyopata kwa kulitangaza jina la Tanzania kimataifa.
Mkwasa alisema kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na nidhamu ya soka aliyokuwa nayo hata kabla ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika.
Alisema alitaka kumkabidhi mikoba hiyo kabla ya kutwaa tuzo hiyo, lakini kiwango kizuri cha Nadir Haroub aliyekichukua kutoka kwa Shadrack Nsajigwa kilimshanya kusubiri.
"Sasa umefika wakati wa kumpa unahodha ili aweze kuiongoza Tanzania," alisema Mkwasa na kuongeza:
"Naamini ataisaidia Taifa Stars kufanya vizuri kama ilivyokuwa kwa klabu yake ya TP Mazembe."
Alisema anaamini chini ya Samatta, Stars itajifunza mambo mengi na kila mchezaji atajitahidi kuiga mafanikio hayo.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment