UDA-RT YASALIMU AMRI VIWANGO VYA NAULI

NA MOSHI LUSONZO

8th January 2016

Mkurugenzi Mtendaji UDA-RT, David Mgwassa
 Kampuni ya Mabasi yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (UDA-RT) imesema haina ugomvi na serikali na kwamba itakubaliana na kiwango chochote itakachoona kinafaa.
 
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, David Mgwassa, alisema kiwango walichopendekeza na kujadiliwa katika Baraza la walaji la Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kisitafsiriwe kuwa ni nauli halali, badala yake inaweza kukubalia au kukataliwa na serikali.
 
Juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alikataa ongezeko la nauli mpya kwa mabasi yaendayo kasi, alisema nauli hiyo itasababisha mzigo kwa wanbanchi na watumishi wa umma.
 
Alizitaka mamlaka husika zikiwemo TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi, Sumatra na UDA-RT kukaa haraka kurekebisha viwango hivyo.
 
Kiwango kilichopendekezwa na UDA ni Sh. 1,200 kwa safari ya njia kuu na Sh. 1,400 kwa njia ya pembeni, wanafunzi watalipa nusu ya kiasi hicho kwa kila barabara.
 
Hata hivyo, Mgwassa alisema kisheria wao walitakiwa kuandaa mchanganuo wa nauli ya utoaji huduma hiyo na kufikisha kwenye baraza la walaji ili wadau watoe maoni.
 
Katika kikao cha kujadili mapendekezo hayo kilichofanyika hivi karibuni, Sumatra  na wadau mbalimbali walipinga nauli hizo wakisema ni gharama kumbwa ambayo wananchi wa kawaida hawawezi kumudu.
 
Sumatra  ilishauri nauli ya usafiri wa kutumia mabasi hayo iwe sh. 400 hadi 500 katika kutimiza malengo ya serikali kusaidi wananchi kuondokana na kero ya usafiri jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Mind 2024

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment